📚 KWAKO BINTI;
✍🏾
' ITAMBUE THAMANI YAKO '
• Huko Duniani Kuna Msemo Fulani Ambao Umejipatia Umaarufu Mkubwa Kidogo,
• Msemo Huo Unazungumzia Habari Ya Kutokukubali kuuziwa Mbuzi Kwenye Gunia,
• Vijana Wengi Wamekuwa Wakiutumia Msemo Huu Kumaanisha Kuwa Hawako Tayari Kuoa Bila Kufanya Zinaa Na Binti...
• Cha Kusikitisha Ni Vile Ambavyo Mabinti Wengi Wameshindwa KUTAMBUA THAMANI Zao Na Kuzishusha Mpaka Kwenye Ngazi Ya Mbuzi!
• Ninasema Ngazi Ya Mbuzi Kwa Sababu Wamekubali Kufanya Zinaa Kwa Kumridhisha Mjinga Mmoja Anayedai Hauziwi Mbuzi Kwenye Gunia..!
• Binti, Unapokubali Kushusha Sketi Kwa Mjinga Anayedai Hauziwi Mbuzi Kwenye Gunia; TAMBUA Kuwa Umeshaishusha THAMANI Yako Mpaka Kwenye Ngazi Ya Mbuzi Jike Mbele Ya Beberu...
• Binti, Ukishatambua Huyo Kijana Anataka Mfanye Uzinzi Kabla Ya Ndoa, Ni Vema Ukajiepusha Na Huyo Beberu Aliyekosea Njia Mpaka Kufika Kwako Mtoto Wa Mungu Uliyenunuliwa Kwa THAMANI Kubwa Pale Msalabani..1Petro 1:18-19
• Binti, Usipoitambua Thamani Yako Uwe Na Uhakika Utageuka Kuwa Uwanja Wa Majaribio Kwa Kila Kijana/Beberu...
• Binti, Ndoa Huwa Haishawishiwi Kwa Kumvulia Kijana Sketi! Ndoa Humfuata Binti Anayeijua Thamani Yake Na Kujitunza!
• Binti, Hata Hao Vijana Waonjaji(Mabeberu), Huwa Wanapotaka Kuoa Huwa Wanawafuata Wale Mabinti Waliogoma Kuwavulia Sketi!!!!
• TAMBUA THAMANI NA UITUNZE!
• Binti, Mtu Asiyeitambua Thamani Yako Hawezi Kuitambua Thamani Hiyo Hata Kama Utampa Thamani Hiyo!
BWANA YESU ALIWAHI KUSEMA JAMBO HILI;
📖Mathayo 7:6
[6]Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, WALA MSITUPE LULU ZENU MBELE YA NGURUWE, WASIJE WAKAZIKANYAGA CHINI YA MIGUU YAO, WAKAGEUKA NA KUWARARUA.
• Maana Yangu Ni Hii; Kama Kijana Anataka Mfanye Zinaa Kabla Ya Ndoa Huyo Hakustahili! Huyo HAKUTHAMINI Na HATAKUTHAMINI Hata Kwenye Ndoa..!
• Kuna Mabinti Wengi Sana Wanaotembea Na Majeraha Yanayotokana Na Mahusiano, Sababu Ya Majeraha Hayo Ni Kuzitupa THAMANI Zao Mbele Ya Nguruwe Na Mabeberu Waliowageuka Na Kuwararua...
• Ukiitupa Thamani Yako Mbele Ya Beberu Uwe Na Uhakika Atakutumia Kutimiza Haja Zake Na Kisha Kuishia Zake!
• Binti Usikubali Kuishusha THAMANI Yako Kiasi Cha Kufananishwa Na Mbuzi! WEWE NI WA THAMANI MNO.!
• Binti Usikubali Kuwa Mbuzi! Hakuna Kijana Ambaye Yuko Tayari Kumuoa Mama Huruma Au Mama Wa Majaribio! Mabeberu Watakutumia Na Kisha Wataenda Kuwatafuta Waliotulia Na Kujitunza..
• WEWE NI WA THAMANI MNO! YESU ALIKUFA KWA AJILI YAKO! WEWE HUNA THAMANI YA MBUZI! WEWE NI MTU..
• IMARISHA MAHUSIANO YAKO NA MUNGU (mathew 6:33), NA MUNGU ATAKUPATIA MTU WA THAMANI KAMA WEWE..
#JITAMBUE
#JITUNZE
#JITHAMINI
- Ahsante Sana Kwa Kunielewa -
# FIKIRI KWA KINA, AMUA KWA BUSARA #
(Ukihitaji Kuwa Miongoni Mwa Wale Tunaowatumia Mafundisho Haya Na Mengine Kwa Njia Ya Wasap Unaweza Kunitumia Ujumbe Kwa Wasap Kupitia Namba Iliyoko Mwishoni Mwa Somo Hili)
Ni
Mimi Ndugu Yako
Edward Godfrey
Whatsapp, 0767054041
©2021, April 24
0 Comments