Advertisement

Responsive Advertisement

SUPER LEAGUE VS UEFA/FIFA/ FA'S

NA GEORGE AMBANGILE ✍

Super League Vs UEFA / FIFA/ FA’s

Nafikiri sasa hizi pande mbili za Super League Vs Mamlaka mengine ya Soka wakae chini na kutafuta suluhisho . Haya mambo haiwezekani yaendelee hivi .

Hii haitakiwi kuhusu nani yupo sahihi Vs nani anakosea , nani anashinda Vs nani anashindwa ...hii inatakiwa ihusu kuokoa soka letu . FOOTBALL SHOULD WIN , waweke majivuno yao pembeni na matumizi ya akili + miiko yatumike

Hawa watu wana upeo sana kujua nini kinahitajika kufanyika, sasa hivi badala ya kuongea kuhusu nini kinatokea uwanjani katika muda muafaka wa msimu, tunaanza kuongea kuhusu nani mbabe ? Nani yupo sahihi ? Nani ashinde ? Nani ashindwe ? Hasa kwenye utawala juu . Come oooon , wapo better zaidi ya hivi .

Ni kweli wamefikia “ a point of no return “ ? kukaa meza moja na kutafuta ufumbuzi wa mchezo wetu pendwa ??? Jinsi ninavyoona wakiendelea kuvutana , kutupiana maneno, kutishiana ...kuna njia moja tu watatupeleka ...,kuharibu FOOTBALL. God forbid . !! Hoja zao , mawazo yao, mipango yao waweke mezani , tafuta suluhisho , faida na hasara, .... bado naamini wanaweza kufanya bila kuharibu FOOTBALL .

Post a Comment

0 Comments