Advertisement

Responsive Advertisement

SHIRIKISHO LA SOKA BARANI ULAYA UEFA LIMETANGAZA KUPITISHA MFUMO MPYA WA MICHUANO YA KLABU BINGWA ULAYA

Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limetangaza kupitisha mfumo mpya wa michuano ya klabu bingwa Ulaya ambayo itakuwa inashirikisha timu 36, ongezeko la timu nne kutoka kwenye mfumo wa sasa. 

Katika mfumo huo unaotaraji kuanza msimu wa 2024/25, michuano itachezwa kwa mfumo wa ligi moja na sio makundi. 

Kila timu itakuwa inacheza mechi 10 dhidi ya timu 10 tofauti katika ligi hiyo (5 nyumbani,5 ugenini) tofauti na mfumo wa sasa kucheza mechi sita dhidi ya timu tatu hatua ya makundi. 

Timu nane zitakazomaliza zikiwa juu kwenye ligi hiyo, zitakuwa zimefuzu hatua ya mtoano ya 16 bora moja kwa moja, na timu zitakazomaliza nafasi ya 9 mpaka 24, zitacheza mechi mbili za mtoano na washindi nane watakaopatikana wataingia hatua ya 16 bora."

Post a Comment

0 Comments