Advertisement

Responsive Advertisement

RAIS WA REAL MADRID FLORENTINO PEREZ AMESEMA VILABU VYOTE VILiVYOJIUNGA EUROPEAN SUPER LEAGUE HAVIWEZI KUONDOKA

 Rais wa Real Madrid, Florentino Perez anasema vilabu 12 ambavyo vilikubali kujiunga na European Super League vina "mikataba ya kisheria" na "hawawezi kuondoka".

- Timu tisa kati ya 12, pamoja na vilabu vyote sita vya Premier, ziliondoka kwenye mashindano yaliyopendekezwa Jumanne baada ya mpango huo kuzua taharuki kali... Ni Real Madrid, Barcelona na Juventus bado hawajaachana na mradi huo.

🗣️ "Sihitaji kuelezea ni nini mikataba inavyofungamana, lakini kwa kweli vilabu haviwezi kuondoka," Perez aliliambia gazeti AS.

🗣️ "Baadhi yao, kwa sababu ya shinikizo, wamesema wanaondoka. Lakini mradi huu upo sawa kabisa, utasonga mbele na natumai hivi karibuni."

- Perez alisema Alhamisi baada ya Arsenal, Chelsea, Liverpool, Manchester City, Manchester United na Tottenham kujiondoa, kwamba ESL bado ipo tu - Klabu za La Liga Atletico Madrid na za Italia AC Milan na Inter Milan pia wamejitoa rasmi, wakati mwenyekiti wa Juventus, Andrea Agnelli alikiri mradi huo hauwezi kuendelea tena.

- European Super League ya timu 12 ilitangazwa Jumapili na kupingwa vikali na tangu wakati huo imesababisha maandamano makubwa nje ya viwanja vya Timu zilizokubali kushiriki huko England.
EuropeanSuperLeague UEFA FlorentinoPerez

Post a Comment

0 Comments