Rais wa Marekani, Joe Biden, amesema kukutwa na hatia kwa ofisa wa polisi aliyemuua, George Floyd ni ushindi, ingawa zinahitajika juhudi zaidi kutokomeza ubaguzi.
Polisi wa kizungu, Derek Chauvin, alinaswa na kamera za CCTV akiwa amemwekea goti la shingo Mmarekani mwenye asili ya Afrika, Floyd, adhabu iliyosababisha kijana huyo apoteze maisha.
Baada ya maandamano ya haoa na pale kulaani tukio hilo, jana Chauvin alikutwa na hatia na huenda sasa ofisa huyo akakumbana na adhabu ya kifungo cha gerezani.
0 Comments