Advertisement

Responsive Advertisement

RAIS SAMIA: NIMEKUJA KULIHUTUBIA BUNGE BAADA YA NCHI YETU KUPITIA KWENYE KIPINDI KIGUMU

“Nimekuja kulihutubia Bunge baada ya Nchi yetu kupita kwenye kipindi kigumu, kama inavyokumbukwa March 17 Taifa letu lilipata msiba mkubwa wa kuondokewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Magufuli,hivyo tusimame kumuombea Mpendwa wetu.
Mapenzi ya Watanzania kwa Hayati Magufuli yalidhihirika katika kipindi cha maombolezo ambapo wengi walijitokeza kumuaga, namshukuru Mungu kwa kutupitisha salama kwenye kipindi cha mabadiliko ya Uongozi, dhamana hii ni kubwa na yenye mitihani mingi.
Kuniamini kwa Hayati Magufuli kuwa Mgombea Mwenza wake kumeniwezesha leo hii kuwa Mwanamke wa Kwanza Tanzania kushika nafasi ya Umakamu wa Rais na hatimaye sasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Niliwahi kusema na leo narudia tena kwamba Mimi na Hayati Magufuli ni kitu kimoja, kwahiyo mengi ambayo nimepanga kuyatekeleza ni yale ambayo yalielezwa na Hayati Magufuli wakati akilizindua Bunge hili" Rais Mhe. SSH

Post a Comment

0 Comments