Advertisement

Responsive Advertisement

RAIS SAMIA: KATIKA MIAKA MITANO TUNAYOKWENDA NAYO TUTAHAKIKISHA KILIMO KINAKUWA NA TIJA


"Kumekuwa na malalamiko mengi kwenye
upatikanaji wa vibali vya kazi kwa wageni, kuna
msemo unasema ukiona mtu mzima analia ujue
kuna jambo, hapa napo kwasababu malalamiko
yamezidi hatuna budi kuliangalia upya jambo hili" 

Rais @samia_suluhu_hassan
"Katika miaka mitano tunayokwenda nayo
tutaendelea kuongeza nguvu kuhakikisha kilimo
kinakuwa na tija, ikiwemo kuwa na mbegu bora,
kuboresha afya ya udongo, pamoja na kuziwezesha taasisi za kilimo kwa kuzipa fedha ili ziweze kuzalisha kwa tija" - Rais @samia_suluhu_hassan

"Kwa miaka hii mitano, tutaendeleza yaliyoandikwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM tutakamilisha ujenzi wa bandari, madaraja makubwa kama ya Kigongo Busisi na Tanzanite, tutaendelea na ujenzi wa reli pamoja na barabara mbalimbali"- Rais @samia_suluhu_hassan

'Kwa upande wa usafiri wa anga tutaendelea kujenga viwanja vya ndege ikiwemo cha kimataifa cha Msalato hapa Dodoma na tutaendelea kulilea shirika letu la ndege ATCL kimkakati ili liweze kujiendesha kwa ufanisi" -Rais @samia_suluhu_hassan Rais Samia Bungeni


Post a Comment

0 Comments