Mkuu wa Wilaya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya amesema Serikali imebaini hujuma zinazofanywa na baadhi ya wafanyabiara wasio waaminifu wanaopandisha bei ya mafuta ya kula na sukari kipindi cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Hatua hiyo nikufuatia malalamiko ya wananchi wa wilaya Hai kwa Mkuu huyo kwamba bei ya mafuta ya kupikia na sukari zimepanda maradufu hali inayolamizu kupika futari na kunywa uji bila sukari huku baadhi ya wafanyabiara hao wakikwepa kulipa kodi ya serikali.
Akizungumza katika mkutano wake wa kusikiliza kero za wananchi uliofanyika katika kituo cha mabasi wilayani humo, Sabaya amesema serikali haitaweza kuwavumilia wafanyabiashara hao huko wakiwaumiza wananchi wa hali ya chini.
@lengai_ole_sabaya amesema uchunguzi wa serikali umebaini mafuta ya kula yapo madukani lakini baadhi ya wafanyabiara hao wamepandisha bei kutoka Sh 22,000 hadi 35,000 kwa lita tano kwa mafuta ya kula.
Amesema baadhi ya wafanyabiara hao wamepandisha bei ya sukari kutoka shilingi 2,500 hadi Sh 3,000 kwa kilo moja ya sukari na hivyo kuwaumiza wananchi was kipato cha chini.
"Nimepitia maduka 11 hakuna wafanyabiashara wanaotoa risiti halali ni kwa sababu siyo bei halali, hivyo hatuko tayari wananchi kuonewa nitaendelea kufuatilia kilio cha wanyonge sitanyamaza kimya katika hili,"amesema Sabaya.
0 Comments