CLASS ...!!!
✍🏼Sikufanikiwa kuangalia kipindi cha kwanza mechi ya Simba Vs Dodoma Jiji kutokana na majukumu ya kazi ( muda huo nilikuwa studio kwenye kipindi cha Sports Court ) lakini kipindi cha pili nilikiona vizuri sana .......niliona nini ???
✍🏼Simba SC walionesha “ Class “ ya hali ya juu kwa dakika kama 15 za kutafuta ushindi halafu baada ya hapo wakatuliza mechi kumaliza dakika ( Game Management ) . Passing , Movements na maamuzi sahihi katika wakati sahihi + Umaliziaji wa umakini sana .
✍🏼Chama , Miquissone, Bwalya , Eresto walivyoanza kupasiania kwa haraka haraka na kwa usahihi, movements zao za kubalishana nafasi ndio ziliwaua Dodoma kwa kipindi cha dakika 15 - 20 . Nafikiri hakuna cha ziada ambacho Dodoma wangeweza kufanya kwa ustadi kama ule . ( siku zote ukipiga sana pasi za mbele na ukiwa na wachezaji ambao wapo tayari kukimbia mbele zaidi / nyuma ya safu ta kiungo na ulinzi ya timu pinzani ni hatari sana ). Vertical passing and Running ahead of the ball.🔥
✍🏼Dodoma Jiji na Mbwana Makata nafikiri wanaweza kuondoka kwa Mkapa kichwa juu , na wametuheshimisha mashabiki wa mpira kwa ujasiri, kujiamini na kuonesha hali ya kupambana uwanjani , walifanya kila kitu kwa asilimia nyingi kwa usahihi, tofauti ni kukosa ubora stahiki kuwaadhibu zaidi Simba SC . Ngumu kujivunia kwasababu umefungwa lakini sioni aibu ya kujivunia kwa mechi nzuri waliyocheza leo. Waliwafikirisha Simba hasa mipira ya kugombania. KONGOLE kwao 👍🏻👍🏻
NOTE :
1: Combination ya Chama Jr na Miquissone ..Aisee daah 🔥🔥 Pasi na Finishing = Class ✅
2: Cleophace Mkandala , utulivu, ufundi , passing ✅🔥
3: Didier amezoeleka : Na Mbwana Makata HESHIMA YAKO KOCHA . Anafundisha mpira kweli
Full Time : Simba 3-1 Dodoma Jiji
0 Comments