Advertisement

Responsive Advertisement

NA GEORGE AMBANGILE "REAL MADRID 1 - 1 CHELSEA"

Vita ya kimbinu

✍🏼Nimeshuhudia timu mbili ambazo zote ziliandaliwa kimbinu kwa ajili ya mechi ya leo , na wachezaji wote walikuwa makini kufuata maelekezo ya walimu . TRUE PROFESSIONALS

✍🏼Jinsi Real na Chelsea walivyokuwa wanachagua wakati sahihi wa kupress juu zaidi kwa idadi nzuri ya wachezaji kwa kuzuia njia ya pasi ( Cutting passing lanes ) na sio kupress kwa kuzuia watu ( Man oriented pressing ) lakini pindi press hiyo ikifeli basi timu zote mbili walikuwa wanarudi haraka sana nyuma kwa idadi kubwa na kujenga “ BACK 5 “ huku wakifunga space baina ya mistari miwili ya mwisho ( Ulinzi na Kiungo ) na kufanya mpira uende kushoto na kulia tu .

✍🏼Pongezi sana kwa Rudiger na Pulisic ( mawasiliano ya macho tu ) Pulisic hakuhitaji kuita kwa pasi bali alimuangalia Rudiger na kukimbia nyuma ya walinzi wa Real ambao walikabia juu . Unahitaji pasi sahihi sana . Niliamini Nacho ndio alikuwa anamuona vizuri Pulisic ili aende naye , kitendo cha kusimama tu ndio goli lilipotokea maana yake Courtois alilazimika kutoka golini na kupigwa chenga .

✍🏼Ujenzi wa mashambulizi kutoka nyuma kipindi cha kwanza , Chelsea walikuwa wafanisi zaidi kuliko Real . The blues wameshazoea kucheza na Back 3 , kwahiyo wanatanua nyuma na Jorginho anatengeneza “ Angle “ ya pasi zote kutoka kwa mabeki wake ..wanafanya uwanja mpana . Real walikuwa karibu karibu sana nyuma na hivyo rahisi kwa Chelsea kupress mpaka kipindi cha pili Zidane akabadilisha na yeye kutanua zaidi uwanja hapo ndio Kroos na Luka wakaanza kupata space kubwa .

NOTE

1: Karim Benzema : Huyu mwamba ni full package . Ana kila kitu 🔥🔥 what a goal

2: Jorginho ni ubongo wa Chelsea sasa hivi . Ndio conductor mwenyewe, sio tu akiwa na mpira bali muangalie anavyoelekeza mikimbio na pasi kwa wenzake

3: KANTENHO na CASEMIRO : wanaiba sana mipira hawa 🔥

Full Time : Real 1-1 Chelsea

Post a Comment

0 Comments