KESHA LA ASUBUHI
Jumatano 28/04/2021
*KITABU KIONGOZI CHA WOKOVU*
*Lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika. Bali wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao.* 2Timotheo 3: 14, 15
📚 Mavumbuzi mbalimbali ya kibinadamu katika kulifafanua Neno, kuwafanya wanafunzi walielewe kupitia hoja za watu walioelimika ni makosa. Mungu hakufanya upokeaji wa injili utegemee mantiki. Injili inapokelewa kama chakula cha kiroho, kutimiza shauku ya roho ya mwanadamu. Ndicho anachokihitaji mwanadamu nyakati zote...
📚 Neno la Mungu ni kitabu kikuu kinachoelimisha. Ingawa wengi wanadai kuliheshimu, bado wanavitanguliza vitabu vingine kabla Yake. Mantiki ya mwanadamu inainuliwa juu ya ile ya Kiungu. Je ni lazima nizungumze kwa uwazi na kubeba ushuhuda niliouamua? Kama Neno la Mungu lingezingatiwa kama lilivyo, kama sauti ya Mungu kwa wanadamu, chanzo cha hekima, kweli, na elimu yote ya juu kwa watoto, vijana na wazazi wangelifanya kuwa siyo tu mtaala wao bali mwalimu wao na kiongozi chao ambacho “katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu.” ( Waefeso 2:7).
📚 "Katika zamani zinazokuja” ni historia gani ambayo zamani hizo zitaifungua. Ni kwa namna gani watoto wa ulimwengu watakavyostahimili kutazama katika urefu na kina cha umilele kilichoitwa na mtume “zamani zijazo”? Ni kitu gani kitakachofahamika kuhusiana na zamani zijazo" ?
📚 Biblia ni kitabu cha kiada, na kinatakiwa kusomwa kwa bidii siyo kama ambavyo tungeweza kukisoma kitabu kimojawapo kati ya vitabu vingi. Kwetu sisi kinatakiwa kuwa ni kitabu ambacho kinakidhi hitaji la nafsi. Kitabu hiki kitamfanya mtu anayekisoma na kukitii kawa mwenye hekima hadi kuupata wokovu. Kama ambavyo chakula hakiwezi kunawirisha mwili bila kuliwa na kumeng’enywa, hata Neno la Mungu aliye hai haliwezi kunufaisha nafsi isipokuwa liwe limepokelewa kama mwalimu katika viwango vya juu vya elimu kama kilicho juu zaidi ya viwango vya kibinadamu; mpaka kanuni zake ziwe zimetiiwa kwa sababu ni hekima ya Mungu...
🔘 *Mungu atalitimiza kusudi lake Mwenyewe, akichukua wakala wa kibinadamu kama mbia mwenza wa mpango imara wa wokovu na kumfanyia yale yote aliyoahidi kulingana na Neno lake “nitafanya wanadamu kuadimika kuliko dhahabu safi, na watu kuliko dhahabu ya Ofiri. ( Isaya 13:12).*
*MUNGU AKUBARIKI SANA*👮♂️
0 Comments