ULISHAJIULIZA MAANA YA NENO "MAMBO MENGI MUDA MCHACHE"
1.Picha linaanza European Super League ikaanzishwa Jumapili tarehe 18/04/2021,mwenyekiti akatanzwa na wasaidizi wake watakaosimamia hayo mashindano
2.Timu 12 zikajiunga kwenye mashindano ya Super League ambazo ni Barcelona,Madrid,Atletico,Man City,Liverpool,Chelsea,Arsenal,Man United,Spurs,Juventus,Intermilan na AC milan tena kwa mbwembwe
3.Viongozi wa nafasi mbalimbali katika shirikisho la soka barani ulaya (UEFA) wakajiuzulu nafasi zao na kuamia super league ukimjumuisha pia Mwenyekiti wa Chama cha Vilabu barani ulaya(ECA), Andrea Agnelli aliyejiuzulu na kuamia Super League ambapo alipewa cheo cha mwenyekiti msaidizi
Kumbuka hayo yote yanatokea Jumamosi, Jumapili na Jumatatu bado hatujafika jumanne😂😂
4.Story zikaenea duniani Rais wa UEFA akaweka msimamo mkali juu ya wachezaji watakaoshiriki ligi hiyo kuwa watafungiwa kucheza EURO na WORLD CUP wakati huo huo taarifa zikawafikia mashabiki Duniani , Kwani mashabiki wenyewe wanasemaje? Wanasema hivi hawataki Super League wala mdogo wake Super League
5.Mara Paap Jumanne ikafika Aprili 20, Rais Wa FIFA,Giano Infantino akasema hayatambui mashindano hayo, kilichotokea baada ya hapo mhhh...
6.Jumanne hapo bado tupo, Mara Man City wamejitoa super league, Chelsea wanajiandaa kuandika barua kujitoa super league, Barcelona wanajiondoa pia wakati huo huo Man Utd muda wowote wanajiondoa, Atletico ndo usiseme walishajiondoa zimebaki timu 7😂😂
7.Ukiachana na timu kujitoa waasi na wenyewe wameanza kujiuzulu, Ed Woodward amejiuzulu nafasi yake ya Mkurugenzi mkuu wa benchi la ufundi wakati huo huo Yuda ambaye ni Andrea Agnelli amejuzulu nafasi yake ya Urais katika klabu ya Juventus
JAMANI ETI HAYO YOTE YAMETOKEA SIJU 4 TUU, JUMAMOSI,JUMAPILI,JUMATATU NA JUMANNE
0 Comments