Advertisement

Responsive Advertisement

MSEKWA AMPONGEZA RAIS SAMIA KUKUBALI KUKUTANA NA VYAMA VYA UPINZANI

Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi, Bara, Mzee Pius Msekwa, amepongeza uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan, kukubali kukutana na Ujumbe wa Vyama vya Upinzani nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam na Waandishi wa Habari wa Uhuru Media Group, Mzee Msekwa amesema hii si mara ya kwanza kwa CCM kukutana na vyama vya upinzani, na kueleza imewahi kufanyika Visiwani Zanzibar, ambapo CCM ilifanya maridhiano na Chama Cha Wananchi-CUF.

Ameeleza kuwa CCM imekuwa na utaratibu wa kukutana na vyama vya upinzani, na kusema nia ni kushirikiana nao katika kuiongoza nchi.

Akizungumzia kuhusu utendaji kazi wa Rais Samia, Mzee Msekwa, amesema ana imani Rais Samia ataendeleza yote mazuri yaliyoachwa na mtangulizi wake Hayati Dk. John Pombe Magufuli aliyefariki Dunia Machi 17 mwaka huu na kuzikwa Machi 26 wilayani Chato Mkoani Geita.

Post a Comment

0 Comments