Miili ya watu 2 na kichwa cha mtu mmoja vimeokotwa kwenye eneo la hifadhi ya Taifa ya Ruaha wilayani Mbarali mkoani Mbeya huku vikiwa vimeharibika na chanzo vifo hivyo kikiwa hakijajulikana.
Aidha kamanda wa polisi mkoani humo Urlich Matei amedhibitisha tukio hilo jana Juma tatu April 26,2021 na kueleza kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi ili kubaini vifo hivyo kama vimetokana na maji ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika eneo hilo au mauaji.
0 Comments