Advertisement

Responsive Advertisement

UMMY MWALIMU: WAZEMBE MTUPISHE

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) , Ummy Mwalimu,  amesema atazifumua Sekretariet za Mikoa endapo hazitatekeleza majukumu yake ipasavyo
Waziri Ummy ameyasema hayo katika kikao cha Sekretariet ya Mkoa wa Tanga iliyoketi katika Ukumbi wa Ofisi  ya Mkuu wa Mkoa  huo
Amesema “Jicho langu la karibu ni Sekretarieti za Mikoa sitaki nianze kupambana na Halmashauri 184 wakati nina watu kwenye Sekretarieti za Mikoa ambao wako karibu kimazingira na kiutendaji na halmashauri hizo ninataka watekeleze majukumu yao ipasavyo na mimi nipate taarifa zote kutoka kwao
Amesema endapo Sekretarieti ya mkoa ambayo atabaini wataalam wake ni wazembe na hawatekelezi majukumu yao ipasavyo itabidi wapishe.

Post a Comment

0 Comments