MFAHAMU ZAIDI PAPA WEMBA(Part3);-Mwaka 1977 Papa Wemba alianzisha Viva La Musica, kundi lililokuwa na wanamuziki takriban 15 ambalo pamoja na mabadiliko ya hapa na pale bado lipo.
Ukubwa wake haukuwa kwenye muziki tu. kwenye viunga vya Kinshasa, Papa Wemba alitengeneza kijiji alichokipa jina “Kijiji cha Molokai” na kujiweka kama kiongozi mkuu.
Ndani ya kijiji hicho alianzisha uvaaji wake. Wakazi wake walitakiwa kuongea kwa namna tofauti, kutembea kivyao. Ulikuwa ni mji uliokuwa ndani ya mji na wenye sheria zake.
Mwaka 1979 aliimba kwa miezi michache na bendi ya Tabu Ley, Afrisa International Orchestra of Tabu Ley na kisha mwaka 1980, alifanya ziara ya Afrika akiwa na santuri ya Analengo iliyouza nakala 60,000.Miaka ya 80 Papa Wemba aliingia mkataba mnono na lebo ya Visa 80 ya Luambo Makiadi, maarufu kama Franco.
Akiwa na safari nyingi za Ulaya alikokuwa akirekodi nyimbo zake, Papa Wemba aling’ara kwa fashion zake na kuwa prince wa jamii ya SAPE (Societe des Ambianceurs et des Personnes Elegantes – Society of Posers and Elegant People).
Mwaka 1983, alienda Ulaya alikokaa kwa miezi minane na kuliacha kundi lake Viva La Musica, chini ya uongozi wa mke wake, Amazon. Kundi hilo liliyumba kutokana na wanamuziki kulipwa ujira kidogo.
Alirejea July 1984 na kulirejesha tena kundi lake kwenye chati. Aliamua kuhamia Ulaya mwaka 1986 baada ya kufanyiwa upasuaji wa jicho lake.
Mwaka 2003 Papa Wemba alifungwa kifungo cha miezi mitatu na nusu jijini Paris kwa tuhuma za kuingiza watu kinyemela nchini humo. Baada ya kutoka jela alikiri kuathirika kisaikolojia na kuamua kuokoka.
October 2003 aliachia albamu yake Somo Trop na kwenye wimbo “Numéro d’écrou”, Papa Wemba anakumbuka jinsi Mungu alivyomtembelea gerezani.
Hadi anafariki, Papa Wemba amesharekodi albamu takriban 43.
0 Comments