MFAHAMU ZAIDI PAPA WEMBA(Part 2):-Katika miaka ya 60, aliimba na vikundi mbalimbali katika mji huo mkuu ambao wakati huo ulibadilishwa jina na kuitwa Kinshasa baada ya kupata uhuru. Kama vijana wengi wa enzi hizo, Papa Wemba alivutiwa na muziki wa Kimarekani na kubadilisha jina lake kuwa Jules Presley.
Mwaka 1969 alikuwa sehemu ya waimbaji waliozalisha kundi lililotamba miaka ya 70, Zaiko Langa Langa. Kundi hilo lilipata umaarufu mapema kwa vijana ambao walianza kuhisi muziki asili wa rhumba ulikuwa wa pole pole mno na uliopitwa na wakati.angu miaka 50, Afrika nzima ilikuwa ikicheza mtindo huu uliokuzwa na Joseph Kabasele na kisha Franco miaka ya 60. Zaiko Langa Langa walikuja na muziki uliochangamka zaidi na Papa Wemba akang’ara mapema na kuliongoza kundi.
Mwaka 1975, baada ya kupata jina, Papa Wemba aliondoka kwenye kundi hilo na kuanzisha kundi lake, Isifi Lokole. Isifi lilikuwa ni kifupi cha Institut de Savoir Idealogique pour la Formation des Idoles (Institute of Ideological Knowledge for the Training
0 Comments