Advertisement

Responsive Advertisement

MFAHAMU ZAIDI PAPA WEMBA PART 1

MFAHAMU ZAIDI PAPA WEMBA(Part1):-Ilikuwa ni Kusini mwa Congo (Zaire kuanzia 1971 hadi 1997 kisha kuwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo) kwenye mkoa wa Kasai ambapo Papa Wemba alizaliwa mwaka 1949. Jina lake halisi ni Shungu Wembadio Pene Kikumba, lakini alipewa jina Papa kwasababu alikuwa mtoto wa kwanza.

Alipokuwa mtoto mchanga, familia yake ilihamia Leopoldville, mji mkuu wa nchi hiyo kipindi cha utawala wa Wabelgiji. Baba yake alikuwa mwanajeshi mstaafu aliyepigana vita vikuu vya pili vya dunia kabla ya kuwa mwindaji.

Mama yake alikuwa muombolezaji mazishi anayelipwa. Kwa kwenda naye mara kwa mara kwenye shughuli hizo, mama yake alimtambulisha kwenye muziki ambao alijikuta akiupenda.
Hata hivyo baba yake alipinga vikali mwanae kuwa mwanamuziki kwasababu alitaka aje kuwa mwandishi wa habari au mwanasheria.

Baba yake Papa Wemba alifariki mwaka 1966. Hakuchelewa na aliamua kuingia kwenye muziki moja kwa moja. Alianza kuimba kwenye kwaya ya kanisa la Mtakatifu Joseph na akatengeneza sauti yake

Post a Comment

0 Comments