Advertisement

Responsive Advertisement

MASHABIKI WA AZAM FC WAWAPIGA CHAI MASHABIKI WA YANGA SC

Mashabiki wa timu ya soka ya Azam jijini Mwanza wamewanunulia kifungua kinywa wenzao wa Yanga kwa kuonyesha mshikamano na furaha ya ushindi wa bao 1-0 waliopata dhidi ya timu hiyo ya mitaa ya Jangwani na Twiga.

Tukio hilo lililivutia umati wa watu limetokea eneo la Stendi ya Igombe jijini Mwanza leo, mashabiki wa Azam wametaja sababu ya kufanya hivyo kuwa ni kuwapoza machungu wenzao wa Yanga ambao baadhi yao walilala njaa bila kula usiku wa kuamkia leo kutokana na huzuni na machungu ya kupoteza mtanange huo wa ligi kuu.

Msosi huo wa bure ulikuwa wazi kwa mwanachama, mpenzi na shabiki yeyote wa Yanga huku baadhi ya vijana wanaoaminika kuwa wapenzi wa watani wa jadi wa Yanga, Simba Sports Club wakizunguka eneo lote la stendi kuwasaka wenzao wa Yanga na kuwasogeza eneo la msosi.

Post a Comment

0 Comments