Advertisement

Responsive Advertisement

DERICK LWASYE: KUHUSU JIMSON MWANUKE NA MESHACK ABRAHAM, TUMEPOKEA OFFER KADHAA ZA VILABU HAPA NCHINI

Habari,Baada ya kupata maswali mengi juu ya wapi ambako watacheza wachezaji Meshack Abraham na Jimson Mwanuke kwa msimu ujao,

Majibu ni kwamba tumepokea Offer kadhaa kutoka kwa vilabu vya hapa nchini ila kwasasa hatuwezi kuvitaja sababu wachezaji wapo katika harakati za kuinusuru timu yao isishuke Daraja hivyo hata wao sijawaambia ni timu zipi zimetuma Offer hizo,

Lengo ni kuwataka wamalize kwanza zoezi zima la kuipambania timu yao ambayo imewatambulisha ligi kuu ili iweze kusalia ligi kuu.

Baada ya ligi kuisha kila kitu kitakuwa wazi .

Ahsante.

By Meneja
Derick Lwasye

Post a Comment

0 Comments