Advertisement

Responsive Advertisement

SIMBA SC v DODOMA JIJI FC LEO MAJIRA YA SAA 1:00 USIKU

SIMBA vs DODOMA JIJI: Leo majira ya saa 1:00 usiku ‘kitaumana’ pale dimbani Benjamin Mkapa, wakati #mnyama Simba SC atakapoikaribisha Dodoma Jiji FC, kwenye kipute cha Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL).

Vijana hao wa mtaa wa Msimbazi, wanaikaribisha Dodoma Jiji huku ikijivunia kunyakua alama zote tisa kwenye michezo yao mitatu ya Kanda ya Ziwa na kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na alama 58, ikicheza michezo 24 Ilianza kuikaanga Mwadui FC bao 0-1, dimbani Kambarage mjini Shinyanga, ikaifuata Kagera Sugar na kuitandika mabao 0-2, dimbani Kaitaba mjini Bukoba. Kisha ikamalizia na Gwambina pale wilayani Misungwi na kuitungua bao 0-1.

Inakutana na Dodoma Jiji ambayo mara ya mwisho kuvaananayo ilikuwa Februali 4, 2021 na Simba ikaibuka na ushindi wa mabao 1-2
Je, Dodoma Jiji itamsimamisha mnyama kwenye wimbi lake la ushindi?

Post a Comment

0 Comments