Kocha Mkuu wa mpya wa Klabu ya Yanga, Nasreddine Nabi amesema hana hofu na mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu zilizopo sasa na kuongeza 'hesabu' zitakamilika vyema katika mechi ya mwisho ya kumaliza msimu wa 2020/21 na si vinginevyo.
"Kwa sasa kila mmoja anajipanga kupata ushindi ili kujiimarisha, huwezi kujua nini kitatokea katika mechi zilizobakia, hakuna ambaye ana uhakika na kile ambacho anakitaka, tutaendelea kujipanga kutafuta matokeo mazuri,"
Baada ya mechi ya jana usiku dhidi ya Azam FC, kikosi cha Yanga kitajiandaa na safari ya kuelekea Sumbawanga kuwafuata Tanzania Prisons kwa ajili ya mchezo wa hatua ya 16 Bora ya mashindano ya Kombe la FA utakaochezwa Ijumaa kwenye Uwanja wa Nelson Mandela.
0 Comments