Advertisement

Responsive Advertisement

MAMBO 10 NA ALI KAMWE "KAGERA SUGAR 0 - 2 SIMBA SC" ✍

Mambo 10 nilioyaona Kagera vs Simba

1: WHAT A GAME.. Pira Futari lililogawanyika kwa vipindi viwili kiwanjani. Dakika 45 za kwanza game ilichezwa kwenye high tempo, Dakika 45 za pili, Tempo ikashuka. Timu zikaanza kugombea kucheza kwa kuuchezea mpira. 

2: Again.. Quality ya wachezaji wa Simba imeamua mchezo. Kwenye modern Football its Time againts Space. Simba wana wachezaji ambao wanahitaji sekunde 5 tu wakiwa na mpira kutumia space kukumaliza.

3: Kocha wa Kagera, Francis Baraza alikuja na system ya 3-4-1-2. Hii ikawa shimo lake la kuangamia. Simba wakatumia kwa haraka spaces zilizoachwa nyuma ya Luhende na Mwaita. Alipoamua kubadilika kwenda kwenye 4-2-3-1 ilishakuwa TOO LATE. 

4: Nimependa sana akili ya kocha wa Simba, Didier Gomes. Alipogundua ameshapata bao 2, akabadili 'style of play' kwa kuishusha tempo ya mechi. Bila shaka Gomes ana 'save Energy' kwa ajili ya CAF na mechi ngumu zijazo za VPL

5: CCHAMA ANAJUA🙌 Msimu uliopita alimaliza na Asisti 10, Msimu huu, Simba wakiwa na zaidi ya mechi 10 kwenye ratiba yake, Amevunja rekodi yake. ASISTI 11 Mpaka sasa. WoW🙌 

6:  Simba inakuwa timu hatari zaidi kiwanjani isipokuwa na mpira kuliko inapokuwa na mpira.. hii ni kwa sababu ya Chama. Anaonekana 'mchezaji asiyekuwa na madhara' Simba ikikosa mpira, wakati huo wapinzani kufunguka na kumpa eneo kubwa zaidi asimame akiwa huru. Huu ni mtego wa Simba. Wanapowin mpira, hawaplay, Wanaattack.

7:  Yule kiungo mkabaji wa Kagera, Abdul Swamad anajua kupiga pasi, ana nguvu lakini ana udhaifu wa kasi. Kwenye system za Baraza na kasi ya Simba kwenye 'Penetration phase', ilikuwa ngumu sana kwake kuidhibiti akili ya viungo wa Simba.

8: Miquissone..🙌 Mahala pakupasia, anatandika haswa. Ni mtu siriaz na mkatili kwa makipa nchini. Vijana wetu wana mengi ya kujifunza kwake.

9: Taddeo Lwanga katika ubora wake wa kukaba eneo na watu🙌 Alipambana na viungo wabunifu sana, akili na mwili wake vimetumika sana kwenye kuilinda Back 4 yake

10: Well done Erick Mwijage. Alipambana na mabeki wagumu sana leo. Ana mengi ya kujifunza kwenye maamuzi ili azidi kuwa mchezaji mkubwa

Nb: Mwambie jirani yako... Yajayo Yanatisha 😀

Post a Comment

0 Comments