NINA JIBU MOJA TU KUHUSU EUROPEAN SUPER LEAGUE. UBINAFSI.
Ninakubali kuwa, vilabu vyote duniani vinahitaji pesa ili kujiendesha. Vilabu vyote duniani vinalenga kutafuta faida. Soka ni Biashara.
Ni kwasababu hii ndiyo maana wazo la Super league limefanyiwa kazi haraka. Vilabu shiriki vitajipatia kipato ' karibia mara mbili ya kipato' wanachopata kwa kushiriki UCL
Ni mpango safi kwa vilabu vikubwa katika nyakati hizi ambazo vilabu vimekubwa na ukata kwasababu ya madhara COVID. Lakini nilikuwa hoja tofauti kidogo.
Ni kweli kuwa bajeti ya Barcelona haifanani na Huesca wala bajeti ya Man United haifanani na Norwich, lakini pia mapato ya Barcelona hayafanani na Huesca na mapato ya Man United hayafanani na Norwich.
Ninachojaribu kukizungumza ni kwamba, vilabu vyote vimeathirika na janga la COVID. Kwahiyo COVID imetumika kama mwamvuli tu wa kujificha kwenye tamaa ya kuvuna mapato makubwa zidi waliyokuwa nayo wakubwa kwa muda mrefu.
Kama alivosema Garry Neville, vilabu vikubwa wamejifikiria wenyewe tu bila kujali madhara yatakayoletwa na UBINAFSI walioupa kipao mbele.
Kama ESL itafanikiwa, maana yake 'gap' la kifedha litazidi kuwa kubwa kati ya vilabu vikubwa na vilabu vidogo. Ushindani utapotea kabisa.
Ligi hazitakuwa na mvuto tena kwasababu ya kupotea kwa ushindani. Kwa mfano ligi kuu ya England, hakutakuwa na vita tena ya kumaliza ndani ya 'top four' kwasababu haitakuwa na maana.
Kama Arsenal,Chelsea, Man United, Liverpool na Spurs watakuwa na uhakika wa kushiriki mashindano ya Ulaya, kwanini wapiganie tena nafasi za juu? Ushindani utabaki kwenye ubingwa tu.
Lakini pia vilabu vidogo vinavopiganiaga kumaliza katika nafasi ambayo itawafanya kucheza mashindano ya Ulaya ili wakutane na vilabu vikubwa, havitakuwa na hizo ndoto tena.
Mwisho kabisa msimamo wangu na matamanio yangu ni kuona wazo la ESL halifanikiwi kwasababu litadidimiza soka kwa kiasi kikubwa.
.
✍@deo_mwanasoka
0 Comments