HERRY MZOZO: ZIMBWE JR. RUKSA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KLABU YOYOTE

Maneja wa Beki na nahodha wa Simba Sc Msaidizi  Mohamed Hussein Zimbwe Jr  Bwana Herry Mzozo Amesema Mkataba wa Nyota Huyo na Simba umebakia Miezi Miwili.

"Mkataba wa umebakia miezi Miwili, Tunasubiria mkataba na Simba uishe, tufanye maamuzi yetu mengine, kama kweli wangetuhitaji tungelimalizana ndani ya miezi sita kama walivyofanya kwa Wachezaji wengine"

Mzozo ameongeza Kuwa 
"Mtu waliyemtuma ndani ya hiyo miezi sita  hatukuelewana naye kwa hiyo akatufanyisha sisi  tufikirie  kwamba mawazo yao ya kizamani sana kwa Sasa Kuna ofa moja mezani hapa kutoka timu kubwa Afrika Kusini, msharahara milioni 23 kwa mwezi pesa ya usajili Randi laki moja na elfu sabini" 

Kuhusu Yanga Kuhusishwa Mzozo Amesema "Mambo ya  Yanga nasikia sikia tu watu wanaanzisha wenyewe wanajijibu wenyewe. Hapa uswahili kwangu sijaona Yanga wakinifuata Lakini hata hivyo  kama Yanga wanataka kutufuata sio dhambi, niwarahishie thamani ya mchezaji ni milioni 100 kwa mwaka ya usajili, mshahara milioni 10 kwa mwezi Ikipungua Millioni 8" - Herry Mzozo, Meneja wa Mohamed Hussein Zimbwe Jr 


No comments