Advertisement

Responsive Advertisement

AMKA NA BWANA LEO

*KESHA LA ASUBUHI* 

JUMATANO, APRILI, 21, 2021
SOMO: *HATIMA YA UMILELE* 

Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima... Kwa ajili ya hayo wengi miongoni mwa wanafunzi wake wakarejea nyuma, wasiandamane naye tena. Basi Yesu akawaambia wale Thenashara, Je! Ninyi nanyi mwataka kuondoka? Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele. Nasi tumesadiki, tena tumejua, ya kuwa wewe ndiwe Mtakatifu wa Mungu. 

 *Yohana 6: 63—69.* 

Neno la Mungu ni mti wa uzima kwa wale wanaotii. Ni neno la wokovu lililopokelewa kwa uzima wa milele. Wale wanaoyafuata mafundisho yake hula mwili na kunywa damu ya Mwana wa Mungu. Matokeo yanayozalishwa na neno hili ndani yetu yanategemeza hatima yetu ya umilele. Lina viashiria muhimu kwa ajili ya kutengeneza tabia sahihi. Mkristo amechaguliwa kuungana na Mungu katika mahusiano ya karibu, maisha yake yameunganishwa na maisha ya Kristo katika uzima wa milele wa Mungu. 

Katika ombi lake zuri Yesu alisema, "Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao." (Yohana 17:20). Hili linawahusisha wote wanaoiamini injili ... "Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.” (mstari wa 21). Umoja na upendo wetu kwa kila mmoja ni utambulisho ambao kwayo tunashuhudia kwa ulimwengu kuwa Mungu alimtuma Mwanawe kuwaokoa wadhambi. 

"Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja. Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.” (Mstari wa 22,23). Kila wakati ninapoisoma kauli hii, ninaiona kuwa ya ajabu sana. Lakini ninaipokea na kuiamini na ninamshukuru Mungu kwa ahadi zake tele anazozitoa kwa masharti kwamba tukidhi viwango vya haki ya Kristo... 

 *Neno la uzima ndilo ambalo Mkristo anaishi kwalo. Kutoka katika Neno hili kila mara tunazidi kupokea ujuzi wa kweli. Tunapata nuru, usafi, wema na imani vinavyofanya kazi kwa upendo na kuitakasa nafsi. Tumepewa ili tukombolewe na kuwakilishwa kama wasio na hatia mbele ya kiti cha enzi cha utukufu wa Mungu. Ushindi wa kustaajabisha alioupata Yesu ni kwa niaba ya mwanadamu!* 

 *BARIKIWA SANA UNAPOTAFAKARI UJUMBE HUU*

Post a Comment

0 Comments