*KESHA LA ASUBUHI*
*Jumatatu 26/04/2021*
*ASKARI WA KIKRISTO*
" _Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani_ ."
Waefeso 6:11
▶️ Bwana atafanya kazi na kila askari wa msalaba aliyejitoa kikamilifu. Lakini hakuna mwanadamu anayeweza kuwa askari mzuri anayefikiri kuwa ni lazima afanye kazi kwa kujitegemea mwenyewe bila watenda kazi wenzake, anayezingatia maamuzi yake kuwa ni bora. Watenda kazi wa Mungu ni lazima waunganishwe pamoja, huyu akitoa kile ambacho mtenda kazi mwingine hana...
▶️ Je tunafanya maandalizi kama ilivyo fursa yetu ya kutufanya kusimama dhidi ya hila za mwovu? Je tunatambua tabia takatifu ya kazi ya Mungu na umuhimu wa kukesha kwa ajili ya nafsi kama watu ambao watatoa hesabu? Ni lazima tuwe macho, “ Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini. Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru. (Warumi 13:11,12).
▶️ Je tunajifunza kuachana na matakwa yetu? Au bado tunaangalia nafsi zetu zaidi kiasi kwamba hata katika kazi na ndugu zetu tunazingatia maamuzi yetu kuwa bora kuliko wote? Mungu anakataza kwamba tusije tukaruhusu kiburi kutuzuilia baraka ambazo Mungu anazitoa kwa wapole na wanyenyekevu. Wale ambao kwa dhati wanamtukuza Mungu wataficha nafsi zao ndani ya Kristo, wakifurahia ikiwa Mungu anaweza kutukuzwa kwa kazi ya wale alioungana nao. Hakuna anayethamini nafsi yake kwa kiwango cha juu atakayeweza kufanikiwa katika kazi ya Mungu. Kadri muda unavyozidi kusonga hisia zake za kujikweza zinaendelea kukua, na punde ataanza kufikiri kuwa ni bora asiungane na wenzake katika kazi bali atapendelea kufanya kazi mwenyewe.
▶️ Hebu tuziweke mbali nasi kila hisia za kujitukuza. Tujiandae kuwa askari bora wa msalaba kwa kujifunza funzo alilolitoa Kristo aliposema "Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu." (Mathayo 11:29).
▶️ *Yeye aliyeyaacha matamanio yote ya kujitanguliza, hakika atatambulika kwa matendo yake yasiyo na ubinafsi. Ili aweze kuwasaidia na kuwatia moyo wengine yuko tayari kuweka kando matamanio yake binafsi, kuwa vitu vyote kwa watu wote ambao kwa namna fulani atawasaidia. Mtu wa namna hiyo ni kiongozi wa kifalme katika jeshi la Kristo.*
0 Comments