Advertisement

Responsive Advertisement

NCHINI GUINEA WATHIBITISHA WATU 7 WAAMBUKIZWA UGONJWA WA EBOLA

Serikali ya Guinea imesema kuwa watu saba wamethibitishwa kuwa wameambukizwa Ebola katika taifa hilo la Afrika Magharibi ambapo watatu kati yao tayari wamefariki dunia. Afisa mkuu wa idara ya Kitaifa ya Afya nchini Guinea Daktari Sakoba Keita alisema baada ya mkutano wa dharura katika mji mkuu wa Conackry kwamba watu saba wamethibitishwa kuwa wameambukizwa Ebola katika taifa hilo la Afrika Magharibi ambapo watatu kati yao tayari wamefariki dunia.

Watu wanne ambao bado wako hai wametengwa kwenye vituo maalum.Idara ya afya ya taifa imesema watu hao walianza kuugua huku wakiendesha, kutapika na kuvuja damu baada ya kuhudhuria mazishi kwenye wilaya ya Goueke. Idara hiyo pia imeongeza kusema kuwa awamu nyingine ya vipimo inaendelea ili kuthibitisha maambukizi hayo ya virusi vya Ebola na wafanyakazi wa huduma za afya tayari wanawafuatilia watu wote waliokutana na wagonjwa hao.

Source: (Dw Kiswahili)
#BinagoUPDATES 

Post a Comment

0 Comments