MUSUKUMA ATOA SABABU ZA YEYE KUOMBA RAISI MAGUFURI AONGEZEWE MUDA

MUSUKUMA ATOA SABABU ZA KWANINI RAIS MAGUFULI AONGEZEWE MUDA

Tuna Soko la Morogoro, Machinga Complex na sasa la Ndugai, wote ni Mashahidi yamefeli, ni Mabilioni mangapi yametumika?,ni kwasababu Wasomi mnashindwa kutafakari kwamba mnapojenga Masoko au Mastendi makubwa ya Mabilioni ile ni huduma na nyinyi mnaweka kama vitega uchumi - Msukuma

Masoko na Mastendi makubwa yanageuzwa vitega uchumi badala ya kuwa huduma, Masikini hawawezi kwenda, hili Jengo la Bunge lilitumia hela nyingi za Watanzania na sisi tungekuwa tunalipia pesa getini ili kuingia humu,tungeona uchungu yale tunayowapangia Wananchi kule chini - MUSUKUMA 

Haya mambo ambayo tunaona Rais ameyafanya tunaweza kuona namna tukamuongezea muda, kwani kitu gani mbona wenzetu wamefanya?, ina maana sisi Watanzania tunaijua Demokrasia zaidi ya Wachina ambao ni Matrilionea?, wamefika mahala wakaona tumuongeze Mtu hata miaka 20 mbele - MUSUKUMA
#BinagoUPDATES

No comments