MASAU BWIRE; HATUKUFUNGWA NA NAMUNGO KWA SABABU YAKUTUZIDI UWEZO, NI KWA SABABU TULIFANYA UZALENDO TUU

BWIRE KUHUSU KUFUNGWA NAMUNGO JANA

Msemaji wa klabu ya Ruvu Shooting @masaubwire amesema Hatukufungwa na Namungo kwa sababu ya kutuzidi uwezo, ni kwa sababu ya uzalendo wetu kwa Taifa, ni matokeo ya kizalendo ya kuwapa morari Watanzania wenzetu kwa ajili ya mechi ya kimataifa inayowakabili.

Kwa uwezo wa kuwafunga tuliokuwanao katika mchezo huo, kama tungewafunga, wangepoteza mwelekeo na morari, hivyo huko Angola ingekuwa aibu, tumeepusha aibu hiyo, kwa kuwajenga kisaikolojia na kuwatia moyo kwamba,  wanaweza, wakapambane.

Kwa uzalendo wetu, tunawapa majukumu mawili Namungo Fc wakayatende huko Angola, mosi, wakapambane, washinde mechi hiyo, pili, wakaitangaze lugha yetu ya Taifa (Kiswahili), kwa kufanya hivyo, uzalendo tuliowafanyia katika mchezo wa VPL, February 7, 2021, utakuwa wa maana. 

Uzalendo kwanza. Tuwaunge mkono wote wanaoshiriki mashindano ya Kimataifa,  ambao kwa msimu huu, ni Simba SC na Namungo Fc.
#BinagoUPDATES

No comments