Advertisement

Responsive Advertisement

mafunzo ya watu wazima leo 14

LESONI, FEBRUARI 14

SOMO: FARAJA KWA SIKU ZA USONI (ISA. 40:1, 2)



Katika Isaya 40:1, 2, Mungu anawafariji watu Wake. Muda wao wa kuadhibiwa hatimaye umekoma. Ni adhabu gani hiyo?



Kuna majibu mengi kwa hili swali. Kulikuwa na adhabu iliyotolewa na Ashuru, fimbo ya hasira ya Mungu (Isaya 10), ambayo kutoka kwayo Mungu aliiokoa Yuda kwa kuangamiza jeshi la Senakeribu katika 701 K.K. (Isaya 37). Kuna adhabu iliyotolewa na Babeli, ambayo ingebeba mizigo na watu kutoka Yuda kwa kuwa Hezekia alionesha utajiri wake kwa wajumbe waliotoka kwa Merodak-baladan (Isaya 39). Pia kulikuwa na adhabu iliyotolewa na moja ya mataifa mengine ambayo dhidi yao Isaya aliandika ujumbe (Isaya 14—23). 



Wakati uo huo, japo “Ashuru” na “Waashuru” wanatajwa mara 43 kuanzia Isaya 7:17 hadi 38:6, taifa hili linatokea mara moja tu katika sehemu yote iliyobaki ya kitabu cha Isaya, ambapo Isaya 52:4 huzungumzia kuhusu mateso yaliyopita toka kwa Misri kisha na “Mwashuri.” Sehemu ya mwisho ya Isaya, ukombozi kutoka uhamishoni Babeli unatajwa (Isa. 43:14; Isa. 47:1; Isa. 48:14, 20), na ni Koreshi, Mwajemi aliyeishinda Babeli mwaka 539 K.K., ambaye atawaweka huru mateka wa Yuda (Isa. 6 44:28, Isa. 45:1, Isa. 45:13). 



Isaya 1—39 husisitizia matukio yanayoongoza ukombozi kutoka kwa Waashuru katika mwaka 701 K.K., lakini mwanzoni mwa sura ya 40, kitabu huruka mbele karne moja na nusu kufikia mwisho wa Babeli, katika mwaka 539 K.K., na kurudi kwa Wayahudi muda mfupi baadaye. 



Je, mada ya kurudi kutoka Babeli inahusishwa na kitu chochote mwanzoni katika Isaya?

Isaya 39 hutumika kama mpito kufikia sura zinazofuata kwa kutabiri utumwa wa Babeli, angalau kwa baadhi ya uzao wa Hezekia (Isa. 39:6, 7). Zaidi ya hayo, utabiri wa Isaya 13, 14, na 21 unahusu anguko la Babeli na uhuru ambao ungeletwa nao kwa watu wa Mungu: “Maana Bwana atamhurumia Yakobo, atamchagua Israeli tena, naye atawaweka katika nchi yao wenyewe.... Tena itakuwa katika siku ile, ambayo Bwana atakupa raha baada ya huzuni yako, na baada ya taabu yako, na baada ya utumishi ule mgumu uliotumikishwa, utatunga mithali hii juu ya mfalme wa Babeli” (Isa. 14:1—4). Zingatia muunganiko wa karibu na Isaya 40:1, 2, ambapo Mungu anawaahidi watu wake kuwa kuna mwisho wa mateso yao. 



Ahadi za Biblia kuhusu mwisho wa mateso zina maana gani kwako sasa, katikati ya mateso yako ya sasa? Imani yetu ingekuwa na uzuri gani bila ahadi hizo? Kwa nini, basi, ni muhimu kuzishikilia, hata iweje?

Post a Comment

0 Comments