LAMINE MORO; NIKO FITI MASHABIKI MSIWE NA HOFU

LAMINE; NIKO FITI WANACHI KUWENI NA AMANI

Nahodha wa Yanga, Lamine Moro amesema afya yake imeimarika na mashabiki wa timu hiyo watarajie kumuona kwenye ubora wake wakati michezo ya Ligi Kuu kwa timu yake itakapoendelea.

Moro alikosa michezo minne ya mwisho ya kumalizia ngwe ya kwanza baada ya kwenda kwao kutibiwa majeraha ya mguu aliyopata kwenye michezo ya ligi.

Ligi hiyo ngwe ya pili inatarajiwa kuendelea Februari 13 baada ya kusimama kwa muda kupisha michuano ya kombe la Mapinduzi na ya kimataifa.

Akizungumza jioni ya leo Moro amesema baada ya kupata majeraha ya mguu aliomba ruhusa kwenda kutibiwa Ghana lakini kwa sasa ni mzima wa afya na yupo tayari kuitumikia klabu yake.

Kwa sasa ni mzima wa afya njema na nipo tayari kuitumikia timu yangu, unajua nilikuwa kwenye kipindi kigumu nilikuwa nasumbuliwa na majeraha sehemu ya mguu lakini baada ya kupata matibabu naona nipo vizuri na madaktari wameniruhusu kufanya mazoezi," alisema.
#BinagoUPDATES

No comments