KAZE ALIPOMUONA CARLINHO ALIONA HAFAI KUCHEZA NAMBA 10

• Kocha Kaze alisema alipomuona mchezaji huyo, aliona hafiti kucheza namba 10.

• Carlinhos alikuwa mzuri zaidi akitokea pembeni, bahati mbaya alipata majeraha na sasa anaendelea vizuri na ameanza mazoezi tayari, alisema.

• Carlinhos ni mchezaji mwenye mbinu sana, anaelewa na anajua, lakini ni mzuri zaidi akitokea pembeni, naamini atafanya kile ambacho mashabiki wanakitarajia kutoka kwake na habari njema kwao ni kwamba amepona na anaendelea vema na mazoezi.

• Nilifanya usajili wa Fiston (Abdul Razak) ili kupata mtu sahihi ambaye ataitendea haki namba 10, mwanzo alijaribu kucheza Carlinhos, Niyonzima (Haruna), Kaseke (Deus) na Farid (Mussa) wote hawakufiti, kwenye nafasi hiyo, alisema.

• Nilitaka mtu mwenye ‘consistency’ walikuepo sawa walicheza, lakini nilitaka ambaye atatupa matokeo mazuri kila siku katika nafasi hiyo, ndiyo sababu wachezaji wanne tofauti walicheza lakini bado kulikuwa na shida.

• Kocha Kaze pia alizungumzia usajili wa Dickson Job: “Job ni mpango wetu wa muda mrefu, ni mchezaji mzuri ambaye amepitia timu ya taifa katika ngazi zote, ana kipaji,” alisema kocha huyo.
#BinagoUPDATES 

No comments