A-Z YALIYOONGELEWA KWENYE PRESS YA SIMBA

• A-Z YALIYONGELEWA KWENYE PRESS YA SIMBA
 
• Kesho utafanyika uchaguzi wa kujaza nafasi ya Mwenyekiti wa Simba wa wanachama. Wagombea wawili ndio watachuana kesho Murtaza Mangungu na Juma Nkamia. Wanachama wanatakiwa kujua hao ndio watawapigia kura”- Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Simba, Boniface Lihamwike.

• Moja ya kigezo cha kupiga kura ni mwanachama kulipia ada ya uanachama hivyo kesho nje ya ukumbi wa mkutano kutakuwa na eneo maalumu ambalo watatumia wanachama ambao hawajalipa kufanya malipo.”- Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa klabu ya Simba, Boniface Lihamwike.

• Mwisho wa muda wa kufanya kampeni ni leo saa 12:00 jioni na baada ya hapo hakuna mtu ambaye ataruhusiwa kufanya kampeni. Kamati inawaasa wagombea kutojihusisha na vitendo vya rushwa.”- Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa klabu ya Simba, Boniface Lihamwike

• Tutaanza mkutano wetu saa 3:00 asubuhi na tunatarajia kumaliza mapema ili wanachama wapate nafasi ya kwenda uwanjani kuangalia mchezo dhidi ya Azam FC. Tiketi za mchezo zitauzwa nje ya ukumbi wa mkutano na vituo ambavyo tumevitangaza - Msemaji wa klabu, Haji Manara.

• Naamini wanachama wa Simba watatumia nafasi yao ya kikatiba vizuri kuchagua Mwenyekiti wa klabu na uongozi wa Simba upo tayari kufanya kazi na yeyote ambaye atachaguliwa kuwa Mwenyekiti - Msemaji wa klabu, Haji Manara.

• Kesho kutakuwa na surprise ambayo tutaitangaza kwa ajili ya timu yetu ya wanawake ya Simba Queens.”- Msemaji wa klabu, Haji Manara. NguvuMoja
#BinagoUPDATES 

No comments