Advertisement

Responsive Advertisement

BAADA YA USHINDI WA GOLI 3 - 0 DHIDI YA TOTTENHAM, GUARDIOLA AANZA NA TAMBO ZA KIBABE

GUARDIOLA AANZA TAMBO MAPEMA 

Baada ya ushindi wa jana wa mabao 3-0 dhidi ya Tottenham, kocha wa Manchester city, Pep Guardiola ameanza tambo mapema kwamba aliwahi kuwaambia watu kuwa kiungo Ikay Gundogan atacheza kama mshambuliaji ila watu walimcheka na sasa kinatokea alichokisema.

Gundogan amekuwa kwenye kiwango kizuri katika michezo ya hivi karibuni, katika ushindi wa jana alitupia mabao mawili, hata hivyo ana mabao 11 katika orodha ya wafungaji bora wa Ligi Kuu England, Mohammed Salah akiongoza kwa mabao 17.

“Nilisema atacheza kama mshambuliaji watu walicheka,”alisema Guardiola. “Naelewa ni kwasababu ana akili ya haraka kufika katika eneo la gol.”aliongeza.

Alisema kiungo Fernandinho alipokuwa majeruhi, Gundogan alikuwa akitumika kama kiungo mkabaji hivyo ilikuwa ni ngumu kucheza eneo la goli la wapinzani.
#BinagoUPDATES

Post a Comment

0 Comments