RAPA DR. DRE BADO YUPO ICU AKIWA YUPO CHINI YA UANGALIZI WA MADAKTARI
Rapa Dr. Dre bado yupo ICU akiwa chini ya uangalizi mkubwa wa Madaktari ikiwa wiki moja baada ya kuugua ugonjwa wa aneurysm ya Ubongo.
Vyanzo vya karibu na Rapa huyo mwenye umri wa miaka 55 vimeiambia TMZ kwamba madaktari wanaendelea kufanya vipimo kadhaa ili kujua nini kilitokea na wamemtaka Dre kusalia ICU ili kufuatilia kwa ukaribu zaidi hali yake.
Katika taarifa yake wiki iliyopita, Dre aliwaambia mashabiki kwamba "anaendelea vizuri" na atatolewa hospitalini hivi karibuni. Alishukuru pia wafuasi wake na Madaktari huko Cedars-Sinai"
Dre alikimbizwa na gari la wagonjwa kutoka nyumba yake ya Pacific Palisades hadi Kituo cha Matibabu cha Cedars-Sinai huko Los AngelesA Jumatatu ya Januari 4.
#BinagoUPDATES
Post a Comment