amka na Bwana
KESHA LA ASUBUHI
Jumatano 13/01/2021
*MAWAKALA KWA AJILI YA MBINGU*
*Neno la mwisho ni hili; mwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu.* *1Petro 3:8*
Ni hitaji kubwa kiasi gani lililopo la kujenga upole na wema. Asiwepo yeyote aonaye aibu kudhihirisha roho ya upole na huruma kwa wale wanaotenda makosa; kwa wale wanaodhani kuwa hawafanyi kosa lolote na wako mbali mno na kutokuwa na makosa mbele za Mungu. Hakuna anayepaswa kufikiri kwamba kudhihirisha huruma ni jambo la kumfanya aone aibu.
Wakati zahama inapokuja katika maisha ya mtu yeyote, na mwingine akajaribu kutoa ushauri, ushauri na nasaha hizo vitategemea mvuto kwa ajili ya wema ambao kielelezo na roho ya mshauri vimekuwa vikiujenga kwake. Ni maisha yenye msimamo, udhihirisho wa mvuto wa dhati kama wa Kristo kwa ajili ya roho iliyo katika hatari, itakayofanya mashauri yatende kazi ya kushawishi na kuileta katika njia salama. *Wale walio wepesi kuwalaumu wengine, wanaozungumza maneno yanayokata na kuchubua mioyo ambayo tayari imejeruhiwa, wanafanya kazi ya Shetani, na ni watendakazi pamoja na mfalme wa giza.*
Hebu nafsi zilizojaribiwa zikumbuke kwamba wakati wanaporudiwa, ni Bwana awezaye kuwaokoa toka mautini. *Hebu roho zinazopokea mashutumu, zikumbuke kwamba, *“wote niwapendao mimi, nawakemea na kuwarudi” (Ufunuo 3:19)*
Wakala wa kibinadamu, akijazwa na Roho ya Kristo, atakesha kwa ajili ya roho kama atakayetoa hesabu. Madai ya Kristo yako juu yetu, na ni lazima tuelewe wajibu wetu na kuufanya katika kicho cha Mungu na jicho likielekezwa katika utukufu wake, na kutokosa uaminifu. Hebu wazo la kibinafsi na hisia za asili zisikumbatiwe ili kufanya vinywa kuwa kimya. *Sema wala usiogope. Moyo ukiwa umejawa upole na upendo kwa ajili ya roho, onya, shawishi, na sihi*.
Kamwe usiache kufanya kazi kwa ajili ya roho ambapo kungali kuna mwali mmoja wa matumaini. *Maneno yako yanaweza kuchoma nafsi. Hivyo kuwa na tahadhari, na kuyavika kwa upendo na upole wa Yesu. Lainisha kila matamshi kwa upendo na huruma*
*Kadiri unavyoshughulika na wengine, kadiri unavyohukumu wengine, vivyo hivyo Bwana atakuhukumu na kushughulika nawe. Hebu wakala anayedai kuwa mtoto wa Mungu, afanyie mazoezi masomo ya Kristo. Ikiwa ana bidii katika kujeruhi, hebu na ahisi wajibu wa kuponya kama wa lazima juu yake. Ukweli ni lazima usemwe katika upendo, na Roho wa Kristo akikaa ndani ya moyo.*
*TAFAKARI NJEMA MUNGU AKUBARIKI SANA MPENDWA*
Post a Comment