JPM; TABORA NDO KILA KITU

"Tabora kuna kila kitu, Tabora ni safi, historia ya Tabora ni nzuri, hata ukitaka wanawake wazuri wako Tabora, ukitaka wanaume wazuri wako Tabora, kwani nasema uongo?, kwahiyo tuitangaze Tabora yetu kwa ajili ya maendeleo na kujenga uchumi" - @MagufuliJP

"Waziri ametoa ombi la wahandisi ambao wamestaafu waongezewe muda, kwa kazi niliyoiona nimeongeza miaka miwili hebu wasimame niwaone wasije wakawa wahandisi hewa, ni mmoja basi awepo hapa au awepo nyumbani nimemuongeza miaka 2 aendelee kufanya kazi "- @MagufuliJP

"Fedha za utekelezaji wa mradi huu ni za mkopo kutoka serikali ya India na India ni marafiki zetu, napenda kutumia fursa hii kuishukuru sana serikali ya India kwa kutupatia mkopo huu, Kaimu Balozi nakuomba utufikishie shukrani zetu" -  @MagufuliJP

"India pia imetupa Dola Mil.500 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji kwenye Miji 28 pamoja na Zanzibar, naamini wametukopesha kwa vile wanajua sisi tuna uwezo wa kulipa, asanteni sana Watanzania kwa kuwa na uwezo wa kulipa madeni tunayoyakopa" - @MagufuliJP

“Tunaajiri Madaktari, mwaka jana niliajiri Madaktari Elfu moja, kumbe Daktari huyohuyo alipofika hapa akanusa tu akaondoka na kuhamia Hospitali binafsi, wakati amesomeshwa kwa fedha zetu, mshahara wetu, kwanini asishtakiwe kwa wizi?”-JPM akiwa Tabora

“Madaktari wanapata mkopo 100%  wakiwa Chuoni, halafu tunawapa ajira Serikalini wanakimbia kisa maslahi, si ungekimbia wakati unasoma?, hela yetu umekula halafu unakimbia kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi, ni kukosa uzalendo”-JPM akiwa Tabora

“Mtafuteni huyo Daktari aliyekimbia Hospitali ya Serikali na hiyo Hospitali binafsi aliyokimbilia, ikiwezekana tunamfungia Daktari, tunaifungia na Hospitali aliyoenda, wakati wa kusomesha hawatuchangii, tukishawasomesha wanakwenda kuwaiba, sio sawa”-JPM,Tabora
#BinagoUPDATES

No comments