CEDRIC KAZE AWATIMUA MASTAA YANGA
Iko hivi kocha Cedrick Kaze aliwapa mapumziko ya siku 10 wachezaji wake kwa sharti moja tu, kwamba walitakiwa kurejea kambini jana. Yaani saa 6:30 ndani ya alama walitakiwa kuwa ndani ya geti la kambi yao iliyopo kule Kigamboni.
Wakati wachezaji wakiwasili baadhi ya mastaa wakakutana na balaa jipya la kuzuiwa kuingia kambini baada ya kufika dakika tano baada ya muda uliopangwa.
Mastaa hao ni kiungo Haruna Niyonzima, Carlos Carinhos, Mukoko Tonomba na kipa Farouk Shikhalo huku mchezaji pekee aliyechelewa na kuruhusiwa kuingia ni beki wao mpya Dickson Job ambaye jana aliwasili kambini hapo kuanza kazi na alikuwa haelewi taratibu za Kaze.
Wamerudishwa unajua kocha hataki masihala na muda na hajali jina lako na wameambiwa warudi walikotoka mpaka atakapowasiliana na viongozi." kilisema chanzo chetu ndani ya Yanga.
Hii ni hatua nzuri kocha anataka kocha anataka kuwaondoa kujisahau baada ya kuchukua kombe, wengine wangeona kama wamemaliza kazi kumbe bado kuna vita kubwa mbele ingawa baadhi wanadai walichelewa kutokana na msongamano wa pale Kivukoni.
Mapema juzi meneja wa Yanga Hafidh Saleh akieleza juu ya ratiba ya kuanza kwao kambi hiyo, alisema hataki kujua mchezaji alikwenda wapi katika mapumziko ya siku 10 walizopewa anachotaka ni saa 6:30 mchana kila mchezaji ambaye alitakiwa kuwasili kambini kuwa humo.
#BinagoUPDATES
Post a Comment