BABU TALE; NAKUMBUKA MKE WANGU AKIWA MUHIMBILI ALIKUWA HALI MBAYA SANA, ALINIAMBIA MIMI NAONDOKA LAKINI NISIOE
"Mke wangu aliniambia nisioe, nakumbuka hiyo siku nimeshinda naye Muhimbili. Akaniambia nimechoka kuishi hii hali, akanishika mkono kuniambia mimi naondoka, lea watoto lakini usioe, usioe, usioe" - @BabuTale
"Mihangaiko yangu mpaka hapa nilipo imechangiwa na Ruge, tuligombana kibiashara tu na maneno ya watu ambao hawakujua kuwa tunagombana kibiashara. Aliniachisha kazi nilikuwa nalipwa milioni 1, akaniambia mshahara hautoshi" - @BabuTale
"Siwezi kusema lolote kwa kwamba watanipa tena baada ya miaka mitano lakini kwa sasa ninachojali ni kupeleka shule, kupeleka maji, kupeleka 'Ambulance' na madawati. Rais Magufuli aliko akae akiwaza kuwa ninamdai barabara"
"Ujana wangu nilio nao mimi sijaenda shule lakini mimi nina 'exposure' kubwa naweza kusema nina Masters ya maisha ya mtaa. Hata Mhe. Rais aliwahi kuniuliza nikamuambia hivyo" -
"Nina mtoto wa nje, siku hiyo nakumbuka tulikwenda kwa Zari Afrika Kusini tukaiona picha mtandanoni, mke wangu akauliza hii ni kweli?, nikamwambi hawa ni wanawake wanaotafuta umaarufu lakini kimoyomoyo nikijua hii ni kweli"
"Haya niliyo nayo sasa ni matunda ya matusi ya hao watu, nikipita mahali hadi napigiwa saluti. Kiukweli nina deni kubwa kwa mke wangu, ninatakiwa nimjengee Msikiti na nimjengee kisima"
"Sijawahi kumblock mtu, sijawahi kumtusi mtu mtandaoni kwa sababu wao wanaonitusi ndiyo wanaonifanya niendeshe gari. Mke wangu niliwahi kumblock kwa sababu alikuwa anapita kwenye akaunti yangu kusoma matusi anakasirika"
"Marehemu mke wangu tulifahamiana Magomeni Kota kwa sababu na yeye alikuwa anaishi pale, nilimtongoza mwaka mzima hajanikubali. Enzi hizo nilikuwa mtu flani rafu halafu yeye ana mambo ya kizungu" - @BabuTale
"Nilipigiwa simu na Rais Magufuli Alfajiri kabla hatujaenda kuzika, tukaongea nikamuambia naona niache kugombea akaniambia Mungu hajaagiza hivyo, maisha ni mapambano na alinitania "wewe Mluguru gani hauko ngangari" " - @babutale
"Kinachoniliza ni kupotez amtu ambaye angeweza kuniongoza kwa vitu vingine, nimepata uongozi lakini yule aliyetakiwa kula good time hayupo" - @BabuTale
#BinagoUPDATES
Post a Comment