Amka na Bwana
KESHA LA ASUBUHI
Jumatatu 04/01/2021
*KULIMA ARDHI*
*Maana kama nchi itoavyo machipuko yake, na kama bustani ioteshavyo vitu vilivyopandwa ndani yake; ndivyo Bwana MUNGU atakavyootesha haki na sifa mbele ya mataifa yote.* I
*Isaya 61:11*
Maneno ya Mungu aliye hai, "Imeandikwa" ni majani ya mti wa uzima, ambayo wanadamu wanapaswa kula ili kupata uzima kiroho. Kadiri tulavyo maneno ya Bwana Yesu Kristo, yanafanyika kwetu uzima wa milele. "Maneno hayo niliyowaambia," Alisema "ni roho, tena ni uzima" (Yohana 6:63). Mkondo muhimu unaohuisha toka kwa Kristo Yesu huponya majeraha yaliyosababishwa na dhambi. Yesu kwetu ni rafiki, hwambiwa haja pia;
Tukiomba kwa Babaye, maombi asikia;
*Haidhuru wengine wanafuata njia gani, imetupasa kutimiza wokovu wetu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. Kwa nini?- Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yetu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema. *Naam, kwa ajili utukufu wa jina lake, hufanya kazi katika akili na mioyo ya wanadamu, walio wa thamani kuu machoni pake, ikiwa watamruhusu kutenda kazi*.
Mtu alipoanguka, Mungu alianza kazi ya kuikomesha mipango ya Shetani. Mungu hufanya kazi ndani ya mtu. "Ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la *Mungu" (1Wakorintho 3:9). Hapo mwanzo Mungu alimpatia mtu jukumu la kulima ardhi. Kazi hii ilifanywa kuwa ngumu zaidi kwa sababu kwa kutokutii mtu alimpa Shetani fursa ya kupanda mbegu za uovu moyoni mwake. Ardhi ambayo hapo awali ilizaa mema tu ikaanza kuzaa magugu, na kukua kwake kukaleta vita endelevu.*
*Kulima ardhi ni shule ambayo mtu aweza kujifunza masomo ya kiroho. Kadiri anavyolima udongo, mtu ataona kama taswira katika kioo kazi ya Mungu katika nafsi ya mwanadamu. Utamaduni wa kiungu huleta ukamilifu. Ikiwa katika muunganiko na Mungu kazi itasonga mbele, wakala wa kibinadamu, kupitia kwa Kristo, siku kwa siku atapata ushindi na heshima katika pambano. Kupitia kwa neema iliyotolewa, atashinda, na atawekwa katika mahali bora. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.*
*MUNGU AKUBARIKI SANA MPENDWA*
Post a Comment