amka na Bwana

KESHA LA ASUBUHI

Alhamisi 31/12/2020

*NAKAZA MWENDO NIFIKILIE MEDE*

*Ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.* Wafilipi 3:13, 14

📝 Mwaka mwingine katika maisha yako unafikia mwisho leo Je, unauonaje? Je umepiga hatua katika mambo ya kiroho? "Umekua kiroho?" Umeisulubisha nafsi yako, pamoja na mivuto na tamaa za mwili? Umeongeza mvuto wa kusoma neno la Mungu? Umepata ushindi wa maamuzi juu ya hisia zako mwenyewe na mielekeo mibaya? Nini kimeandikwa katika rekodi ya maisha yako kwa mwaka ambao sasa unapita milele na ambao hautakumbukwa tena?

📝 Unapoingia katika mwaka mpya, hebu uwe na azimio la dhati kusonga mbele katika maisha haya ya kiroho, Hebu maisha yako yainuliwe zaidi na kuadilishwa kuliko yalivyo. Fanya lengo lako lisiwe kutafuta raha na kujifurahisha mwenyewe, bali kuendeleza kazi ya Mkombozi wako.

📝 Usibaki katika nafasi ambayo wewe mwenyewe daima utahitaji msaada, na ambapo wengine watahitajika kukuongoza katika njia nyembamba. Unatakiwa uwe imara kutoa mvuto mtakatifu kwa wengine. Unaweza kuwa pale ambapo shauku ya moyo wako itaamshwa kutenda mema kwa wengine, na kuwafariji wenye huzuni, kuwatia nguvu walio dhaifu, na kubeba ushuhuda wa Kristo popote unapopata fursa ya kufanya hivyo. Lenga kumheshimu Mungu katika kila jambo, kila wakati na kila mahalia beba imani yako katika kila jambo.

📝 Jiandae kwa ajili ya umilele kwa jitihada ambazo hujawahi kuzionesha. Ifunze akili yako kuipenda Biblia, kupenda mikutano ya maombi, saa ya tafakari ya kina ya mambo ya kiroho, na, juu ya yote, saa ambapo unakuwa katika ushirika na Mungu. Akili yako inapaswa kujazwa mawazo ya kimbingu kama unahitaji kuungana na kwaya ya mbinguni katika majengo mazuri kule Juu...

🔘 *Ukurasa mpya unafunuliwa katika kitabu cha kumbukumbu za malaika... Hebu kumbukumbu zinazoandikwa humo zisiwe zile zitakazokuaibisha zitakapofunuliwa katika kusanyiko la wanadamu na malaika.*

*MUNGU AKUBARIKI SANA*👮‍♂️

No comments