Amka na Bwana

KESHA LA ASUBUHI

Jumatatu 28/12/2020

*PAZIA LITAFUNGULIWA*

*Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi yafumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso.* 1Wakorintho 13:12

🔷 Pale, ambapo pazia ambalo hutia giza uono wetu litakapoondolewa, na macho yetu yatautazama uzuri wa dunia ambao sasa tunauona kwa sehemu kupitia hadubini; tunapoutazama utukufu wa mbinguni, ambao kwa sasa tunauona kwa mbali kupitia darubini; pale ukungu wa dhambi utakapoondolewa, dunia nzima itaonekana katika uzuri wa Bwana Mungu wetu, ni nyanja ya namna gani itafunuliwa katika kujifunza kwetu!

🔷 Hapo wanafunzi wa sayansi wataweza kusoma rekodi za uumbaji, na kutambua kuwa hakuna taarifa inayokumbusha sheria ya uovu. Watasikiliza muziki wa sauti za asili, na kugundua kuwa hakuna sauti ya kulia au ya huzuni. Katika vyote vilivyoumbwa watagundua mwandiko ulioandika —katika ulimwengu wote tazama "Jina la Mungu linatawala,"  katika dunia, bahari au mbingu, ishara mojawapo kwamba anaishi...

🔷 Historia isiyo na ukomo na ya utajiri usioelezeka itakuwa wazi kwa mwanafunzi. Hapa, kutoka katika ufunuo wa neno la Mungu, mwanafunzi ataweza kuona uwanja mpana sana wa historia, na wataweza kupata maarifa ya kanuni ambazo huongoza mwenendo wa matukio ya kibinadamu. Lakini maono yake bado yamefunikwa na wingu na maarifa yake hayajakamilika. Mpaka pale atakaposimama katika nuru ya milele ndipo atakapoona mambo kwa uwazi mkamilifu...

🔘 *Pazia lililopo kati ya dunia ya yanayoonekana na yasiyoonekana litafunguliwa na mambo ya kustaajabisha yatafunuliwa... Pale wote ambao wamefanyakazi kwa roho zisizo na ubinafsi wataona matunda ya kazi zao. Matokeo ya kila kanuni njema iliyofuatwa na tendo lolote la uaminifu yataonekana... Matokeo ya kazi ya uaminifu katika maisha haya hapa duniani yataonekana kuwa madogo kiasi gani kwa watendaji! Wazazi na walimu wakiwa wamelala katika usingizi wao wa mwisho, kazi yao ya maisha yote ikionekana kuwa bure; hawajui kuwa uaminifu wao umefungua chemchemi za baraka ambazo hazikomi kutiririka, na mvuto wao ukijirudia mara elfu... Hapa tendo na mwitikio vyote vitaonekana.*

*TAFAKARI NJEMA SANA*👮‍♂️

No comments