SIMBA TUMEJIPANGA CHAMA HAWEZI KWENDA YANGA
Simba tumejipanga, Chama hajaenda popote, tushasaini nae mkataba atabaki na Simba hadi 2022 kwa hiyo hoja ya Chama tuimalize. Tumemalizana na Chama na ni mchezaji halali wa Simba”-Mohamed Dewji moodewji"
Chama anamapenzi na Simba na ni mchezaji mzuri ambaye ameshakuwa mchezaji bora wa Ligi na ameshinda tuzo nyingine nyingi. Hatuwezi kuruhusu watu watuwahi”
Chama tulishamalizananae muda mrefu lakini hatukutaka kutangaza, tulitaka kuja kutangaza rasmi lakini kuna propaganda zimezidi kwa hiyo tunataka kuwatuliza mashabiki wa Simba ndio maana tumetoka na kutangaza”
Hatuwezi kutamka kiasi gani tumemlipa kwa sababu tumekubaliana hatutasema sehemu yoyote, kwa hiyo nikisema kesho Chama anaweza kuipeleka Simba mahakamani kwa sababu imekiuka makubaliano”
#BinagoUPDATES
Post a Comment