MSIMAMO WA YANGA KUHUSU TUHUMA ZA SIMBA SC KWA YANGA

MSIMAMO WA YANGA KUHUSU TUHUMA ZA SIMBA KWA YANGA
 
Kwa Mijibu Wa M/kiti wa yanga Dokta Mshindo Msolla;"

Senzo Mazingiza aliitwa kituo cha Polisi kwa madai kwamba alihusika na kupanga matokeo"

Yanga imesikitishwa na kitendo cha klabu ya Simba kufikisha kesi hii Polisi kwasababu masuala ya mpira wa miguu na changamoto zake yalitakiwa kufikishwa Katika Mamlaka zinazosimamia mpira wa miguu, na hii ni kwa msingi wa Utawala bora, halikupaswa kupelekwa Polisi"

Kifupi Yanga wamesikitishwa kwa kuhusishwa na Upangaji wa matokeo, lakini wanaimani kwamba wenye mamlaka watatoa miongozo na kusimamiwa"

Pia wwenyekiti wa Yanga Dokta Mshindo Msolla amesema suala hilo sio suala la mtu binafsi,bali ni la Taasisi"

Kama kuna klabu haijaridhishwa na hili, unapaswa kufuata utaratibu na wao Yanga wapo tayari kutoa ushirikiano kwa ajili ua maslahi ya Mpira wa Nchi"

Dokta Msola Amesema Suala La Upangaji Matokeo Sio Sifa Mbaya Kwa Klabu Tu Ya Yanga, Bali Kwa Taswira Nzima Ya Mpira Wa Tanzania."
#BinagoUPDATES
.

No comments