Mchungaji Mgogo azichambua wizara mbela ya Magufuli

Dar es Salaam. Mchungaji wa Kanisa la Baptist Tanzania, Daniel Mgogo amemwomba Rais John Magufuli kuzisimamia wizara zake ili ziweze kufanya kazi kwa ushirikiano na kuepusha watu kubomolewa nyumba zao kutokana kujenga katika maeneo yasiyostahili.

Ameyasema hayo leo Jumatano Septemba 4, 2019 katika mkutano wa mashauriano baina ya Rais Magufuli na watumishi wa Bodi ya usajili wa Makandarasi (CRB), Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) ambao unafanyika jijini Dar es Salaam.



Amesema wananchi wamekuwa wakiumizwa na vitendo vya kubomolewa nyumba zao ili kupisha ujenzi wa barabara jambo ambalo lingeweza kuzuilika endapo wizara zingeshirikiana.Mtu amejenga katika eneo la barabara, anaomba umeme anawekewa umeme, anaomba maji anawekewa, leo tena unakuja unaniambia ulikosea na inabomolewa, hii inaonyesha kuwa kama vitu vikifanyika kwa utaratibu mzuri itawasaidia wananchi,” amesema Mchungaji huyo huku akishangiliwa na wataalamu hao wa ujenzi

No comments