Mchungaji adaiwa kutengeneza mchawi feki

Kushoto ni RPC Iringa, Juma Bwire na kulia ni mama anayedaiwa kuwa Mchawi, Magreth Simon.

Mchungaji Jeremiah Charles mkazi wa Ilula mkoani Iringa, aliyezua gumzo hivi karibuni mara baada ya mwanamke aliyedaiwa kufanya mambo ya kishirikina kuganda juu ya nyumba yake, ameeleza kushangazwa na taarifa zinazoeleza kuwa mchawi huyo alilipwa pesa ili afanye kimbwanga hicho

''Wale polisi kazi yao ni polisi, mimi ni mtumishi na mtumishi anafanya kazi ya kiroho na wao wanafanyakazi ya Serikali, haya mambo ya kiroho watayajua upana wake kivipi, mambo ya imani wanayajua watumishi, mimi ndo najua kwamba, imani yangu nilivyoomba Mungu ndiye aliyejibu, kwahiyo wao kama wamefanya uchunguzi ni wa kibinadamu, mimi ninachokijua katika ulimwengu wa kiroho kuna vita kati ya Shetani na Mungu, na nguvu ya Mungu siku zote itabaki kuwa juu.'' amesema Mchungaji Jeremiah.

Tukio hilo la mwanamke kukutwa juu ya paa akiwa amevalia mavazi meusi na ungo, lilitokea mwishoni mwa mwezi wa Agosti, ambapo Jeshi la Polisi Iringa lilimshikilia mwanamke huyo kwa ajili ya mahojiano na siku ya jana ya Septemba 3,2019 ilitoa taaarifa iliyoeleza udanganyifu uliofanywa na mwanamke huyo, ikiwemo ukweli wa tukio lenyewe pamoja na majina na mkoa aliotoka.

Chanzo-EATV

No comments