Msanii wa nyimbo za injili Kenya Afariki dunia

Leo ya tarehe 31/08/2019
Msanii wa nyimbo za injili Audrey Chibole, maarufu kama Audrianna, amefariki.
Audrianna, ambaye alikuwa na miaka 22, alifariki baada ya kuugua saratani ya maini kulingana na taarifa kutoka kwa mamake.
Ni baada ya kusafirishwa mpaka hospitali ya Nairobi ambapo aligunduliwa alikuwa na saratani ya maini.

Wasanii mbali mbali wamekuwa wakituma rambirambi zao kwa familia kutokana na kifo cha nyota huyo.

Source: Tuko

No comments