Waumini 25 waokolewa kanisani, baada ya kufichwa ndani na Mchungaji
Jana tarehe 03 July 2019 huko kagera, Mkuu wa wilaya ya Karagwe bwana GODFREY MWALIKWA; Alifanya oparesheni ya kushitukiza katika kanisa moja, na kukuta waumini waliofungiwa ndani kwa siku kadhaa wakiwa hali mbaya NA wengine mahututi kutokana na kuombewa huku wakipigwa fimbo usiku na mchungaji huyo ili wapokee miujiza!Mkuu wa wilaya aliwanusuru mahuhuti hao kwa kuwakimbiza hospital ya wilaya ya karagwe kwa AMBULANCE!
Naomba na wakuu wa mkioa/wilaya nyingine Tanzania fuatilieni nyendo za haya makanisa bubu ni kero kwakweli! Msiwaogope hawana madhara kwenye siasa kwasababu kwanza huwa hawapigi kura siku za jumapili wako busy!
Msipo wapiga marufuku ipo siku sisi wanajamii tuishio karibu na makanisa tutajichukulia sheria mkononi tuwapige manati usiku wanapotupigia kelele na spika zao za disco.
Post a Comment