Padre na sista wafariki dunia

Ajari Kilimanjaro leo yaua watu:
Watu wawili wamefariki dunia kwa ajali wilayani Mwanga, Mkoani Kilimanjaro mara baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugonga gari la mizigo lililokuwa limeegesha kando ya barabara.Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo Julai 4, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah, amesema ilitokea majira ya jioni katika barabara ya Kichwa Cha Ng’ombe eneo la Mgagao wilayani humo.

Alisema gari hilo aina ya Toyota Land Crus lenye namba za usajili T 234 AHY likitokea Lushoto likiwa na abiria wawili ilifika katika eneo hilo na kuligonga kwa nyuma gari namba T 647 SMC na kusababisha vifo vya abiria hao papohapo.

Aidha aliwataja waliofariki katika ajali hiyo ni dereva, Padri Aminiel Chrstopha (47) mkazi wa Wilaya ya Lushoto na mtawa (sista) Oktavian Richard (51) mkazi wa wilaya ya Rombo na kwamba chanzo cha ajaili hiyo ni mwendeokasi alikuwa nao dereva.

No comments